Image
Image

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI MATARAWE ILIYOKO SONGEA AVAMIWA NA MAJAZI.


Na. Mwandishi Wetu.
 
WATU wanaosadikiwa  kuwa ni majambazi wamemvamia mwalimu wa shule ya Msingi Matarawe iliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma kwa lengo la kumpora fedha alizokuwa nazo kwenye mkoba wake wakati akirejea nyumbani kwake kutoka kwenye shughuli zake za kikazi na ujasiriamali.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 28 mwaka huu majira ya saa 1.30 usiku katika eneo hilo la Matarawe wakati mwalimu Rehema Mgeni(35) ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki katika soko la Manzese mjini Songea ambaye hufanya biashara hiyo kwa kushirikiana na wafanyabiashara wengine wa samaki.
Deusdedit Nsimeki - Kamanda wa Polisi Ruvuma.
Alisema kuwa mwalimu huyo ambaye hufanya biashara kwa kushirikiana na wafanyabiashara wadogo wadogo ambapo hukusanya fedha zao kwake na yeye huagiza samaki kwa kiwango kikubwa na baada ya mzigo huo kufika Songea hugawawia kulingana na fedha walizotoa.

Hata hivyo katika  siku hiyo ya tukio mwalimu Mgeni alikuwa ameshakusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara wenzake wa samaki na kuondoka kuelekea nyumbani kwake kwa kutumia usafiri wa gari dogo na alipofika nyumbani kwake alivamiwa na kundi la watu zaidi ya watatu wakiwa na silaha na kumuamuru awape fedha alizokuwa nazo lakini yeye aliwajibu watu hao kuwa hana fedha ndipo walipofyatua risasi hewani kitendo kilichomfanya mwalimu huyo aangushe mkoba aliokuwa nao.

Wakati kitendo hicho kikiendelea mtoto mdogo wa kiume wa mwalimu huyo alifanikiwa kuuchukua mkoba wa mama yake uliokuwa na fedha na kukimbia nao chumbani na kujificha nao chini ya uvungu wa kitanda huko sebuleni juu ya meza kukiwa na mkoba mwingine unaofanana na ule wenye fedha na watu hao waliamua kuingia ndani na walipouona mkoba huo waliuchukua wakiamini kuwa ndiyo ule wenye fedhalakini baada ya askari polisi kufika eneo hilo mtoto huyo alijitokeza akiwa na mkoba wa mama yake wenye fedha.

Kamanda Nsimeki alisema kuwa hakuna mti yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi unaendelea kuwasaka watu hao ambao inadaiwa walikuwa na silaha aina ua SMG au SAR kufuatia ganda la risasi lililokutwa katika eneo hilo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment