Image
Image

EXCLUSIVE: WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WATAKIWA KUANGALIA MFUMO UNAOTUMIKA KUJADILI BAJETI YA SERIKALI NA KUZINGATIA MAZINGIRA YA SASA IWAPO UNAKIDHI MAHITAJI YA WAKATI HUU.

Changamoto imetolewa kwa wabunge kuangalia mfumo unaotumika kujadili bajeti ya serikali ambayo imekuwa ikijadiliwa kila mwaka kwa wakati na utaratibu ule ule, licha ya wabunge kupata fursa mbalimbali za mafunzo kuhusu mifumo mbadala ya bajeti.

Aidha wametakiwa kutathimini kama mfumo unaotumika ni endelevu kwa kuzingatia mazingira ya sasa na kama unakidhi mahitaji ya wakati huu.

Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ametoa changamoto hiyo wakati akifungua mafunzo ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za kudumu za bunge, yanayolenga kuliwezesha bunge kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia na kuishauri serikali kwa ufanisi zaidi
ANNE MAKINDA - SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA.

Amesema kutokana na mfumo huo bunge limekuwa likiweka mkazo katika matumizi ya bajeti bila kuishauri serikali nini cha kufanya ili kuhakikisha bajeti ya matumizi inayopitishwa bungeni inatumika kama ilivyokusudiwa pamoja na kuishauri serikali katika kupanua wigo wa ukusanyaji wa kodi na kuwabana wakwepa kodi.

Awali mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali Ludovick Uttoh, ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo chini ya ufadhili wa benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB), amesema mafunzo hayo ni sehemu ya kujaribu kuelewa kwa pamoja hali ambayo imekuwepo kwa muda mrefu na namna inaweza kupata ufumbuzi unaofaa ili kuwa na mfumo unaoendana na wakati uliopo.

LUDOVICK UTTOH - MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI( CAG)
Kwa kutambua umuhimu wa kuboresha mfumo wa bajeti nchini Bunge litakuwa na ofisi ya bajeti ambayo italiwezesha Bunge kushauri kikamilifu kwenye mchakato wa bajeti ya serikali katika hatua zote na kufuatilia utekelezaji wake kwa karibu huku pia ikiwa mbioni kuanzisha kamati ndogo ya kuishauri serikali kuongeza mapato yake.

Mafunzo hayo ya siku mbili pamoja na mambo mengine yataangalia masuala muhimu ya kibajeti yaliyojitokeza katika ripoti ya CAG, tathimini ya utekelezaji wa bajeti kwa mtizamo wa ofisi ya taifa ya ukaguzi na kutolewa kwa mapendekezo ya kuboresha mfumo wa bajeti ya Tanzania
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment