Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu limetakiwa kutenga fedha kulingana na vipaumbele vya ofisi ili kuboresha huduma inayotolewa na ofisi hiyo katika kuratibu na kusimamia shughuli za serikali.
Aidha menejimenti imetakiwa kulishirikisha Baraza la wafanyakazi pamoja na wafanyakazi katika maandalizi ya bajeti katika hatua za awali kabla hata ya ukomo wa bajeti kutolewa na hazina ili kuondoa malalamiko ambayo yanaweza kujitokeza mara baada ya maamuzi ya vikao vya juu.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Bw. WILLIAM LUKUVI alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa ofisi ya waziri mkuu ambapo amesema kuwa Baraza la wafanyakazi ni chombo cha kuimarisha na kuboresha demokrasia mahala pa kazi, demokrasia aliyoielezea kuwa ni mfumo unaoweka wajibu na haki za kila mwajiri na mwajiriwa katika kufanikisha malengo ya kiuchumi na kijamii.
Bw. WILLIAM LUKUVI - WAZIRI WA NCHI OFISI YAWAZIRI MKUU |
Waziri Lukuvi ametoa changamoto kwa ofisi ya waziri Mkuu ambayo ndio wasimamizi wakuu wa matumizi ya fedha za serikali kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha za umma ili bajeti ya serikali iliyopangwa itumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Ametahadharisha inapotokea migogoro miongoni mwao ni vyema kutafuta suluhu ya kudumu na pale inaposhindikana basi migogoro hiyo ifikishwe katika ngazi za juu kwa ajili ya usuluhishi
0 comments:
Post a Comment