Akizungumza katika Mkutano huo, Makamu wa rais wa TCCIA Bw. ISAAC DALLUSHI amesema vikwazo vya kibiashara vimekuwa changamoto kubwa ya wafanyabiashara katika kutekeleza majukumu yao.
Akitoa mfano amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imeanzisha mfumo wa kutoa risiti katika mashine , mfumo ambao umekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara kutokana na mashine hizo kuwa na matatizo ambapo risiti hazionyeshi namba ya TIN na hivyo kuiomba serikali ifuatilie suala hilo.
Mkutano huo umetanguliwa na warsha inayohusiana na vizuizi vya biashara kuhusiana na suala zima la Soko la pamoja nla Afrika Mashariki.



0 comments:
Post a Comment