Image
Image

P- FUNK - NITAHAKIKISHA KILAKITU KINAKWENDA SAWA KWENYE MSIBA WA NGWEA.

Producer maarufu na mkongwe nchini Tanzania hasa  katika muziki wa bongo P-Funk Majani ameonyesha ni namna gani alivyoguswa na kifo cha msani Albert Mangwea aka. KAOBAMA, NGWEA, COWBOY na majina lukuki aliyokuwa nayo mwanamuziki huyo, ambapo mwandaaji huyo wa muziki  amesema hilo nipigo ambalo kamwe hatolisahau.

P - FUNK ni Mwandaaji pekee  wa muziki nchini Tanzania ambaye alishiriki kwa kiasi kikubwa kuweza kuhakikisha marehemu  Ngwair  enzi za uhai wake kutambulika katika game ya muziki wa Bongo Flava.

Kauli hiyo aliitoa mbele ya waandishi wa habari  Leaders Club jijini Dar es Salaam, ambapo alielezea utayari wake katika kushirikiana vyema  na familia, ndugu, jamaa,  marafiki, na wanamuziki wenzake,hadi hapo marehemu Albert Mangwair,  atakaopopumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.
HII NI SAUTI YA P- FUNK BOFYA HAPO.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment