Wasanii wa bongo movie nchini Tanzania wameungana na wasanii wezao wa muziki wa kizazi kipya katika kuomboleza kifo cha msanii maarufu Hip-hop Albert Mangwea kilichotokea nchini Afrika Kusini alikokuwa kikazi.
Akizungumza huku akionekana mwenye huzuni mwenyekiti mstaafu wa bongo movie Jacob Stephen maarufu kwa jina la JB amesema wameupokea msiba huo kwa huzuni kubwa juu ya kufariki kwa msanii Albert Mangwea a.k.a. MIMI kwa kuwa ameacha pengo kubwa kwa wasanii wa bongo fleva hususani wa miondoko ya hip-hop na Bongo fleva .
|
JACOB STEPHEN JB- MWENYEKITI MSTAAFU BONGO MOVIE |
Kwaupande wake mayasa mrisho amesma ameguswa mno na msiba wa msanii huyo kikubwa ni kumuombea dua.
|
MAYASA MRISHO - MSANII WA BONGO MOVIE |
|
MAREHEMU MANGWEA - KIPANDE HIKI NI KATIKA NGOMA ALIYOKUWA WAMESHIRIKIANA KUIMBA NA FID Q |
Katika kuonyesha kuguswa zaidi na msiba huo msanii wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura maaarufu kama lady JD ama lady anaconda ameshindwa kuzungumza na vyombo vya habari hali iliyomfanya Gadna G Habashi ambaye ni mume wa msanii huyo kuzungumzia juu ya uamuzi wa lady JD kuahirisha tamasha lake lililokuwa lifanyike tarehe 31 mwezi huu hadi hapo baadaye ili kuwapa nafasi wapenzi wake kuomboleza msiba huo.
|
GADNA HABASHI - MUME WA LAD JAYDEE. |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment