Wanamuziki wa Bongo Fleva,muziki wa dansi,ndugu jamaa na marafiki wamekutana kwa dharura jijini Dar es Salaam na kuunda kamati itakayoratibu na kusimamia urejeshwaji wa mwili wa aliyekuwa mwanamuziki wa bongo fleva Albert Mwangwe aliyefariki jana nchini Afrika Kusini.
Kamati hiyo inayoongozwa na kaka wa marehemu Kenneth Mangwea inaundwa na wanamuziki na wadau wa muziki akiwemo Adam Juma ambaye ni msemaji mkuu wa kamati hiyo,Profesa Jay,Lady Jay D,Khalfa Majan maarufu kama P Funk,TID,JMO na Mchizi Mox.
Akizungumzia kuhusu kurejesha mwili wa marehemu nyumbani kwa ajili ya mazishi Juma amesema msiba wa marehemu utakuwa Mbezi Goig Jijini Dar es Salaam ambapo kamati itawajibika kukusanya michango chini ya usimamizi wa familia ya mwanamuziki huyo na pia watafanya mawasiliano na watu wa Afrika Kusini kuhakikisha kwamba mwili wa marehemu unarejeshwa mapema kwa ajili ya kupumzishwa.
|
ADAM JUMA - MSEMAJI WA FAMILIA. |
|
WASHIRIKI KATIKA KUPANGA MIKAKATI YA MAZISHI. |
|
JMO NA WASANII WENGINE WAKIWA WAMESIMAMA KILA MMOJA AKIWAZA LAKE JUU YA MSIBA WA RAFIKI YAO. |
|
MWANA FA (KULIA) AKIWA NA WATU WENGINE KATIKA ENEO LA KUHANI MSIBA KILA MMOJA AKIHUZUNIKA KWA STYLE YAKE. |
|
MCHIZI MOX( KULIA) NA P FUNK ALKIYEVALIA T SHETI NYEKUNDU WAKIWA WAMEKAA KATIKA ENEO HILO LA NYUMBANI KWA MAREHEMU. |
|
JMO ALIYEVAA KEPU NA LAD JAY DEE(KULIA) AKIONEKANA MWENYE HUZUNI BAADA YA RAFIKI NA MTU WAKARIBU ALIWEHA KUFANYA KAZI NAYE KUFARIKI DUNIA. |
Baadhi ya wanamuziki wa bongo fleva na Dada wa mwanamuziki huyo Liloty Mangwea wameelezea kuhuzunishwa na kifo cha ghafla cha msanii huyo kwa kuwa mbali ya kuwa alikuwa na kipaji cha aina yake pia alikuwa nembo ya muziki huo hapa nchini na kwamba kazi zake kamwe hazitaweza kusahaulika.
|
LILOTY MANGWEA - DADA WA MAREHEMU |
|
BAADHI YA WANAMUZIKI WAKIWA ENEO LA NYUMBANI KWA MAREHEMU MANGWEA WAKITETE JAMBO. |
|
ISPECTOR HAROUN - MWANAMUZIKI TANZANIA, |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment