Na. Mwandishi Maalum.
AMILIA ya msanii Albert Mangwea aliyefariki dunia jana nchini
Afrika Kusini, imeanza taratibu za mazishi na jioni hii inafanya kikao Leaders
Club, Kinondoni, Dar es Salaam.
Nyota wa Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Ngwair,
alifariki dunia jana jioni akiwa nchini Afrika Kusini kutokana na kuzidiwa
na matumizi ya dawa za kulevya.
Wakati mwili wake unakimbizwa hospitali ya St
Hellen Joseph, rafiki yake naye, msanii pia M To Te P alikuwa katika hali
mbaya, pia kwa utumiaji wa dawa za kulevya ambako hadi sasa amelazwa kwa
matibabu na taarifa zinasema anaendelea vizuri.
Kaka
wa marehemu Ngwair, Kenneth Mangwea amesema msiba upo Mbezi Beach, Goigi mjini
Dar es Salaam na taratibu za kuirejesha miili ya marehemu nyumbani zimeanza.
Kimuziki,
Ngwair aliibukia mkoani Dodoma ambako alikuwa katika kundi moja na Dark Master,
Noorah na Mez B na amekuwa akishirikiana na M To The P tangu akiwa msanii
anayechipukia baada ya kuhamia Dar es Salaam.
Baada ya kuja Dar es Salaam,
Ngwair akapata dili Bongo Records chini ya mmiliki wa studio hizo, Petter
Matthysse ‘P Funk’ aliyemuinua zaidi kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa
wanamuziki nyota nchini.
Wimbo wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003
ambao ulimpatia umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka
2003 ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake.
Hata hivyo,
mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya,
hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa usanifu na kuanza taratibu
kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo gari aina ya Jeep.
Ngwair kutoka
kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam akajikuta anarejea
kuishi katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam.
Mwaka
2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu kumuinua
tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na kumuwezesha kutoa
albamu ya pili, Nge.
Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi
kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za
kulevya na ‘kuharibika zaidi’.
Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya
Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005.
Mwaka 2003,
msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka na CD ya wimbo
Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho alichowashirikisha Mchizi Mox
na Ferooz.
Ngwair alijaribu sana kumuinua kimuziki M, lakini pamoja na ukweli
kwamba alikuwa ana kipaji, lakini hakufanikiwa, ingawa aliwahi kutoa albamu
0 comments:
Post a Comment