CHAMA cha
Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku Tanzania kimeiomba serikali kutunga sheria ya
kudhibiti matumizi ya tumbaku inayoendana na matakwa ya Mkataba wa Kimataifa wa
Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku ili kuzuia madhara yanayoendelea kutokea kwa
wananchi wasiotumia na wanaotumia tumbaku.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Kudhibiti
Tumbaku Tanzania Bi. Lutgard Kokulinda Kagaruki wakati akitangaza maadhimisho
ya siku ya kutokumia Tumbaku Tanzania yatakayofanyika Mei 31 mwaka huuna
kuongozwa na kauli mbiu isemayo Piga Marufuku Matangazo, Promosheni na
Ufadhili wa Tumbaku.
“Baada ya
kutambua kuwa madhara ya tumbaku ni janga la dunia, Shirika la Afya Dunia
lilipendekeza Mei 31 ya kila mwaka iwe Siku ya Kutotumia Tumbaku
Duniani na kuielimisha jamii juu ya madhara ya afya yanayosababishwa na
matumizi ya tumbaku” amesema Bi. Kagaruki.
Akizungumzia
tafiti zilizofanywa na taasisi mbalimbali kuhusiana athari za matumizi ya
tumbaku Bi. Kagaruki amesema kuwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road mwaka 2010 ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 32 ya saratani zote
zilihusishwa moja kwa moja na matumizi ya tumbaku na kuigharimu serikali zaidi
ya dola za kimarekani milioni arobaini kuhudumia wagonjwa wa saratani.
Magonjwa
mengine yanayohusishwa na matumizi ya tumbaku ni pamoja na magonjwa ya moyo,
kisukari, upungufu wa nguvu za kiume, vidonda vya tumbo pamoja na magonjwa sugu
ya kifua.
Aidha Bi.
Kagaruki amesema kuwa muendelezo wa matangazo, promosheni na ufadhili wa bidhaa
za tumbaku Tanzania umesababisha ongezeko kubwa la matumizi ya tumbaku miongoni
mwa vijana ambapo utafiti uliyofanywa mwaka 2008 na Global Youth Tobacco Survey
unaonyesha kuwa asilimia 10.6 ya wanafunzi wanatumia bidhaa zinzotokana na
tumbaku.
Naye
mkulima wa Tumbaku kutoka Tabora Bw. Salum Rajabu Matongo amesema kuwa tumbaku
ni zao linalomwezesha kupata fedha kwa ajili ya kuhudumia familia yake lakini
ni zao lenye athari nyingi zikiwemo kudhoofisha mwili wa mtumiaji, kusababisha
madhara mengi kama uharibifu wa mazingira kutokana na kukata miti wa ajili ya
kukausha tumbaku na kuathiri macho kutokana na moshi.
0 comments:
Post a Comment