SERIKALI imesema kuwa
itachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi nafasi yake katika jamii
kufuatia kuwepo kwa watu wachache wasiyoitakia mema
nchi yetu kutaka kupandikiza chuki za kidini miongoni mwa Watanzania na
kuleta mapigano, mauaji nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo
Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati
akitoa kauli ya Serikali kuhusu mlipuko wa uliotokea katika kanisa
la katoliki la Mtakatifu Joseph Parokia ya Olasiti Arusha
mjini Mei 5, mwaka huu saa 4:30 asubuhi na kusababisha vifo vya
watu wawili na kujeruhi 59, kati ya hao watatu ni mahututi.
Aliwataja watu
waliofariki dunia kuwa ni Regina Kurusei mwenye wa miaka 45 mkazi wa Olasiti
ambaye alifariki siku ya tukio wakati alipokuwa kipatiwa matibabu katika
hospitali ya Mount Meru na James Gabriel(16) aliyefariki usiku wa
kuamkia leo.
“Tutachukua hatua kali
bila huruma kuzigandamiza njama hizi mbaya dhidi ya taifa letu.
Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi na nafasi yake
katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza,” alisema Waziri
Nchimbi.
Alisema tayari
kikosi kazi maalumu kimeundwa ili kuchunguza tukio hilo.
Waziri Nchimbi
alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mlipuko huo ni bomu. Hivyo
uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika unaendelea kufanywa na
Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania .
“ Hadi sasa
watuhumiwa sita wanashikiliwa na jeshi la polisi. Miongoni mwao ni Victor
Ambroce mwenye umri wa miaka 20, dereva wa bodaboda,mkazi wa Mrombo,
Arusha,ambaye anatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. Watuhumiwa wengine watano
waliokamatwa ni raia wane wa kigeni na Mtanzania mmoja ambao
wanashikiliwa kwa maahojiano,” alisema.
Aidha Waziri Nchimbi
alisema Serikali inamewataka wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na
kauli zinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki
miongoni mwa Watanzania.
”Serikali isilaumiwe
kwa hatua kali za kisheria itakazozichukua dhidi ya viongozi wa aina hii
ambao maslahi yao ni muhimu kuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu
kuliko umoja wa Watanzania,” alisisitiza huku akisema Serikali kwa nguvu zake
zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wote waliohusika na kushiriki kwa namna
yoyote katika tukio hilo wanasakwa popote walipo na kufikishwa katika
vyombo vya sheria..
Aliongeza kuwa kwa niaba
ya Serikali anaungana na Watanzania kulaani wahusika wote wa tukio hilo
walioshiriki kwa njia yoyote. Pia inawataka viongozi wa kisiasa,
kidini,na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika ili
kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu.
Mlipuko huo ulitokea
muda mfupi baada ya kuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia,
mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Baba Mtakatifu, Askofu Fransisco Mantecillo
Padilla. Aidha alikuwepo mwenyeji wake Askofu Josephat Lebulu wa Jimbo
Kuu la Arusha.
Inakadriw a kuwa katika
uzinduzi huo kulikuwa na watu zaidi 2000. Hivyo wakati mgeni rasmi akiwa
ametoka nje akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi
mtu aalirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na
mkusanyiko wa watu na baada ya kutua kulitokea kishindo na mlipuko mkubwa.


0 comments:
Post a Comment