Image
Image

EXCLUSIVE: BAJETI YA MWAKA 2013/ 2014 VINYWAJI SIGARA NA NA MAGARI CHAKAVU ZAPANDA KWA KIWANGO TOFAUTI


Wabunge wakitafakari Bajeti wakati ikisomwa leo.
Serikali imetangaza marekebisho ya sheria za kodi kadhaa ikiwemo ya mapato na ushuru ambapo, kodi za bidhaa mbalimbali zinazozalishwa hapa nchini na kutoka nje kama vinywaji, sigara, nishati ya mafuta na magari zimepanda kwa viwango tofauti.
Dk,William Mgimwa
Akiwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Bungeni leo, Waziri wa Fedha Dk,William Mgimwa amesema lengo ni kuongeza mapato ya ndani na kupunguza uingizaji wa magari chakavu na kulinda viwanda vya ndani vinavyozalisha samani.

Waziri Mgimwa amesema kodi ya mafuta ya Dizeli imepanda kwa kiasi cha shilingi mbili kwa lita kwa kutambua kwamba magari makubwa na mitambo mbalimbali inatumia mafuta hayo katika shughuli mbalimbali.
James Mbatia ( kushoto) na Waziri mkuu mizengo Pinda wakijadiliana mambo kadhaa wakati waziri mgimwa akiendelea kusoma bajeti kwa mwaka 2013/ 2014 - Bungeni mjini dodoma leo.
Aidha, kodi ya Mafuta ya Petroli imepanda kutoka shilingi 300 hadi 400 kwa lita huku, kodi ya mafuta ya taa ikibaki bila ongezeko lolote.
James Mbatia ( kushoto) na Waziri mkuu mizengo Pinda wakijadiliana jambo wakati bajeti ikiendelea kusomwa leo, wengine wanao onekana ni baadhi ya wabunge wakifuatilia kwa umakini.
Mh. Bernad Membe( kulia) akionekana kuteta jambo. 
Akizungumza kodi ya mapato ya ajira, Waziri Mgimwa amesema Serikali imepunguza kodi hiyo kutoka asilimia 14 mpaka 13 hatua ambayo itakuwa nafuu kwa wafanyakazi.
Mh. Mbowe (kushoto) na john mnyika (katikati) zitto kambwe  mwishoni, wakonekana kutafakari bajeti kwa dizaini tofauti Bungeni Mjini Dodoma Leo
Katika bajeti hiyo ya mwaka wa fedha 2013/14,Serikali inakusudia kukusanya shilingi trilioni 18.2 kutoka vyanzo vyake vya ndani nje ikilinganishwa na bajeti ya mwaka iliyopita na kwamba na bajeti hiyo inazingatia vipaumbele vilivyoanishwa katika mpango wa maendeleo wa mwaka  2013/2014 na mfumo mpya wa utekelezaji wa vipaumbele vyenye matokeo makubwa na ya haraka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment