Image
Image

MSAFARA WA TIMU YA IVORY COAST KUWASILI JIJINI DAR ES SALAAM KWAAJILI YA MCHEZO WAKE WA MARUDIANO NA TAIFA STARS.


Msafara wa timu ya taifa ya Ivory Coast "The Elephants" watu 80 wakiwemo wachezaji 27 unatarajiwa kuwasili nchini usiku huu kwa ndege maalum kwa ajili ya mechi ya marudiano  dhidi ya Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars kwa jili ya kusaka tiketi ya kushiriki kwenye fainali ya Kombe la dunia mwakani nchini Brazil.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Boniface Wambura,kikosi hicho cha Ivory Coast  ambacho kitawasili bila ya nyota wake Didier Drogba  kitafikia kwenye hoteli ya Bahari Beach iliyopo nje Kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kitaondoka saa chache baada ya mechi hiyo ya Jumapili.
Boniface Wambura
Mchezo huo  utakaochezeshwa na Mwamuzi kutoka Algeria utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili saa tisa alasiri ambapo tiketi zitaanza kuuzwa keshokutwa ambapo kiingili cha chini kitakuwa ni shilingi 5000 kwa viti vya rangi ya kijani.


Baadhi ya wachezaji nyota wanaounda  timu hiyo ni pamoja na Mwanasoka bora wa Afrika Yaya Toure,Tiote Cheik,Arouna Kone,Salomon Kalou,Seydou Doumbia na Sio Giovanni.

Wakati Ivory Coast ambayo inaongoza kwenye kundi C wanawasili leo,Taifa Stars ambaye imeweka kambi kwenye hoteli ya Tansoma inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Wakati huo huo makocha wa timu zote mbili Taifa Stars na Ivory Coast watakutana na Waandishi wa Habari Jumamosi kwenye makao makuu wa TFF 
 





Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment