Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi,
amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka saba jela, baada ya mahakama ya mjini
Milan kumtia hatiani kwa kosa la kumlipa mtoto kwa ajili ya ngono.
Hata hivyo habari zinasema kutokana na uwezekano wa
rufaa mbili zilizopo, inaweza kuchukua muda wa miaka kadhaa kabla ya hukumu ya
mwisho kutolewa.
Silvio Berlusconi
Imeripotiwa kuwa mawakili wa bw. Berlusconi
wanakusudiakukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo waliyoieleza kwamba haieleweki na
ina lengo la kumchafua kisiasa mteja wao.
|
Jopo la mahakimu watatu, ambao wote walikuwa wanawake,
pia lilimtia hatiani bw. Berlusconi kwa kosa la kutumia vibaya mamlaka yake,
kutokana na waziri mkuu huyo wa zamani kuandaa mpango wa kuwezesha kuachiwa kwa
msichana mdogo aliyemlipa kwa ajili ya ngono, alipokamatwa na polisi kutokana
na tuhuma za wizi.
0 comments:
Post a Comment