Serikali imeongeza viwango vya fedha zinazopelekwa
kwenye halmashauri nchini kwa ajili ya malipo ya likizo za walimu ili
kuwawezesha kupatiwa fedha hizo.
Kassim Majaliwa - Naibu Waziri wa TAMISEMI |
Wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa
imewaagiza maafisa elimu nchini kuandaa mapema orodha ya walimu wanaotarajia
kwenda likizo ili kuwawezesha walimu hao kulipwa fedha za likizo.
Akizungumza kutoka Bungeni mjini Dodoma Kupitia TBC Naibu
waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa amebainisha hayo katika kipindi cha maswali
na majibu leo bungeni mjini Dodoma, ambapo amesema maafisa elimu wanatakiwa
kuandaa orodha hiyo miezi miwili kabla ya walimu kwenda likizo ili kutayarisha
mchakato wa malipo.
Cue in ... Kassim Majaliwa - Naibu Waziri wa TAMISEMI
0 comments:
Post a Comment