Image
Image

EXCLUSIVE: DREVA BODA BODA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUINGIA CHINI YA UVUNGU WA GARI, GEREJI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM.


Jeshi la polisi kitengo cha usalama bara barani kimeombwa kuwachukulia hatua askari wake wa usalama bara barani wanao ondoka maeneo yao ya kufanyia kazi na kwenda kupiga soga mtaani na kusababisha ajali zisizo za lazima kutokea.

Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wananchi punde tu baada ya kutokea ajali iliyohusisha  dreva boda boda kunusurika kupoteza maisha kutokana na kuingia uvuguni mwa gari baada ya kugongwa wakati akiwa na haraka ya kumwahisha abiria wake ili awahi kurudi na kuchukua abiria mwingine.

Wananchi hao katika maelezo yao ni kile wanachodai kuwa endapo angekuwapo askari wa usalama bara barani huenda isinge tokea ajali hiyo, kwani madreva hao wamekuwa wakiendesha kwa kasi mno chombo hicho cha moto, hivyo kuomba askari hao wanapo wakamata dreva hao wakiwa mwendo kasi wawachukulie hatua zitakazo kuwa ni funzo kwa wengine.



SHUHUDA WA AJALI HIYO AKIWA ANAANGALIA HALI ILIVYO BAADA YA AJALI.
BWANA JAMALI DREVA WA BODA BODA AKIWA KAKAA HUKU AKITAFAKARI MAJERAHA ALIYOYAPATA KWENYE MWILI WAKE, BAADA YA KUINGIA UVUNGUNI MWA GARI AINA YA TATA NAKUUMIA HUKU AKIANGALIA PIA PIKIPIKI YAKE ILIYOO HATUA CHACHE NA ALIPO ILIISIJE KUIBIWA NA WATU WATUKUTU AKAPOTEZA KABISA.
BAADHI YA WANANCHI PAMOJA NA DREVA WA GARI LILILOGONGANA NA BODA BODA WAKINYANYUA BODA BODA HIYO, BAADA YA KUGUNDUA KUWA MWENYE MAKOSA NI DREVA WA BODA BODA ALIYECHOMEKEA GARI HILO.
ALIYEVAA BLUE NI DREVA WA GARI ILIYOGONGANA NA PIKI PIKI HIYO, AKIZUNGUMZA NA DREVA WA BODA BODA BWANA JAMALI NA KUMUULIZA KAUMIA WAPI KUSUDI AMPELEKE HOSPITAL YA AMANA KABLA YA HAJAZIDIWA.
BWANA JAMALI DREVA WA BODA BODA AKIONYESHA MAJERAHA ALIYOYAPATA BAADA YA KUGONGWA NA GARI HIYO NA KUINGIA CHINI YA UVUNGU HUO.
NAMBA YA GARI IKIWA INAONEKANA VIZURI.
HAYA NDIO MAANDISHI YALIYOKUWA KWENYE GARI LILILOGONGANA NA BODA BODA ILALA  MSAADA GEREJI JIJINI DSM.

MWANA BLOG MR SEMVUA AKIFUATILIA HATUA KWA HATUA, JINSI AJALI HIYO ILIVYOTOKEA NA HATMA YA MWENDESHA BODA BODA NA MAJERAHA ALIYONAYO.
DREVA WA GARI AINA YA TATA AKIZUNGUMZA NA DREVA WA BODA BODA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA JAMAL, KUHUSIANA NA AJALI HIYO NA HATIMA YAKE, NA MWISHOE WAKAMALIZANA KIKUBWA BILA ASKARI WA USALAMA BARA BARANI KUFIKA.
MBELE YAKO HAPO NI DREVA BODA BODA ALIYEVALI HELMENT, ALIYEVAA TAI NI MR SEMVUA MSANGI WAKATI AKIPATA MAELEZO KWA KINA NA KULIA HAPO NI MWENDESHA BODA BODA AKIELEZEA AJALI ILIVYOKUWA HADI MWENZIE AKANUSURIKA KUPOTEZA MAISHA.
PICHA HIYO INAONYESHA JINSI ILIVYOKUWA AJALI HIYO, NA HAPO ZIKIWA ZIKIONEKANA NAMBA ZA USAJILI ZA GARI HILO LILILOGONGANA NA BODA BODA HIYO.

HILI NDILO GARI LILILOGONGANA NA BODA BODA, HAPO BODA BODA IKIONEKANA IKIWA CHINI BAADA YA AJALI HIYO ILIYOTOKEA MSAADA GEREJI ILALA JIJINI DSM MUDA MUDA HUU.
BW.MREMA (KUSHOTO) MR SEMVUA (MSANGI KULIA)  NA AMBAYE NI MMILIKI WA BLOG HII AKIWA KASIMAMA KA STAILI YA AINA YAKE AKIWA AMEVALIA TAI NYEUSI BAADA YA KUPATA PICHA ZA AJALI HIII.
HII NDIO PIKI PIKI ILIYO INGIA CHINI YA GARI HIYO, HAPO ZIKIONEKANA NAMBA ZAKE.

Hata hivyo eneo hilo la ilala gereji kumekuwa kukitokea ajali za mara kwa mara hasa zinazo sababisha watoto kupoteza maisha na hata watu wazima kutokana na kutokuwekwa matuta ikizingatiwa bara bara hiyo imenyooka kutoka mjini hadi buguruni ilalala.

Aidha dreva wa boda boda Bw. Jamali ameumia sehemu mbali mbali za mwili wake huku mguu wake ukielezwa huenda hata ukawa umevunjika kutokana na kuwa umeumia vibaya na kushindwa kuendesha tena pikipiki.

Madreva hao wote waliongea na kuelewana huku dreva wa gari akijichukulia jukumu la kumsaidia dreva wa boda boda kwa kiasi chochote cha fedha kwa lengo la kujiuguza na kuahidi kumtengenezea pikipiki yake, ingawaje makosa yakiwa kwa mwendesha boda boda kwa kupita bila kufuata sheria za bara barani.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment