Wadau wa soka mkoani Tabora wamekumbushwa umuhimu wa kuwasaidia vijana katika michezo ili kutekeleza dhana nzima ya michezo ni ajira hatua ambayo pia itawawezesha kupunguza kero ya ukosefu wa ajira kupitia sekta muhimu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa mstahiki Meya wa manispaa ya Tabora kwa ajili ya Jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM kata ya Kiloleni,mjumbe wa kamati ya uchumi na fedha jumuiya ya Wazazi mkoani Tabora ambaye pia ni mlezi vijana Chipukizi,Emmanuel Mwakasaka ametoa rai hiyo huku akiwataka vijana kutopuuza michezo na kuifanya kuwa ni suluhisho la ukosefu wa ajira.
![]() |
| PICHA NA MAKTABA YETU. |
Aidha Mwakasaka
pamoja na kuzungumzia
masuala hayo ya
michezo alitumia fursa
hiyo pia kuwaasa vijana
kutojihusisha na vitendo
vinavyoweza kuathiri maisha
yao huku wakiwa
bado taifa linawategemea
katika masuala mbalimbali
ya kiuchumi.
| PICHA NA MAKTABA YETU. |
Kwa upande wake
mstahiki Meya wa manispaa
ya Tabora Ghulam
Dewij amempongeza kada
huyo wa CCM
huku akiwataka wadau
wengine wa maendeleo
ya michezo mkoani
Tabora kujitokeza kwa
wingi kuiga mfano
huo kwa kusaidia
michezo ya aina
mbalimbali na si kushia katika
soka pekee.


0 comments:
Post a Comment