Migogoro
ndani ya vyama na vilabu vya michezo nchini inaweza kuepushwa iwapo viongozi na
wadau wa michezo kukubali kufanya kazi kwa pamoja katika kudumisha amani,umoja na mshikamano kwa maslahi ya
umma.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu wa mafunzo wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Raphael Matola,wakati wa mahafali ya kumi na saba ya chuo cha Diplomasia Dar Es
Salaam ambapo yeye alikuwa ni kati ya wahitimu 641 waliotunukiwa vyeti katika
ngazi mbalimbali ikiweno cheti,stashahada na Shahada baada ya kufuzu mafunzo
mbali katika Diplomasia ya kimataifa.
Mwanamichezo
huyo,amesema mahusiano mema ni hatua ya kupiga hatua za maendeleo kwenye sekta ya
michezo kwa kuwa inaondoa mifarakano na migogoro baina ya jamii na kuliwezesha
taifa kusonga mbele.
Aidha Matola,ametoa wito kwa wadau wote wa mchezo
wa soka nchini hususani wale wanaodai kile kinachoitwa haki,kuheshimu maagizo
ya shirikisho la soka duniani FIFA,kutaka masuala ya soka kumalizikia kwenye
soka na si kwingineko.
0 comments:
Post a Comment