Watangazaji
hawa wenye kiu na ndoto ya kufika mbali hasa katika sekta hii ya utangazaji,
uandaaji na mambo mengine mengi katika tasnia hii wamesema kwa sasa wanaandaa
maandalizi ya kufungua radio yao huko mkoani mwanza.
Akizungumza
na Blog hii Mkurugenzi wa KATORO
FM RADIO Bw. Abeli mussata amesema Radio hiyo kwa sasa ipo katika
hatuaza mwisho kwani mambo mengine tayari yamekamilika hivyo vijana wenye kiu
na ndoto ya kuwa watangazaji wakae mkao wakula kwani Radio hiyo itakuwa Mkombozi
kwa vijana kujikwamua wenyewe kimaisha.
ABEL MUSSATA - MKURUGENZI WA KATORO FM RADIO |
Bwana Mussata amewaasa vijanawanao hitimu
masomo yao katika vyuo mbali mbali vya uandishi wa habarinchini Tanzania kuacha
tabia ya kuchagua sehemu ya kufanyia
kazi, bila kufikiria Muda na umri vinasogea na havirudi nyuma.
" Vijana wengi sasa hivi wanashindwa
kufikia lengo kutokana na kuwa wengi wanang"ang"ania kutangaza radio
kubwa za hapa mjini Pasipo kuwa nauzoefu wa radio ambayo ndio chipukizi hivyo
unakuta wanasota bila chochote kupata na baadae akisha stuka umri unakuwa umekwenda"
alisema Abeli.
Hata
hivyo amesema kuwa ameamua kupeleka mwanza KATORO FM RADIO kutokana na
hapa mjini kuwa na ushindani mkuubwa wa radio changa na zinazo anza.
Amesema uamuzi wa kuifungua mwanza ni nafuu
kwani baada ya miaka kadhaa itakuwa pia hadi usikivu wake unafika Karibia Tanzania
nzima.
Aidha
ameongeza kwa kusema kuwa wiki hii anarudi tena mwanza baada ya kukamilisha
baadhi ya taratibu za radio hiyo na kuwahakikishia uma kwamba mwezi wa nane
mwaka huu itakuwa tayari inasikika, kwa baadhi ya maeneo ya kanda ya ziwa na kwingineko.
0 comments:
Post a Comment