Ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za
Sekondari Tanzania (UMISSETA) kanda ya Kusini Mikoa ya Lindi na Mtwara
umefanyika rasmi katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lindi.
Akizindua Mashindano hayo yatakayotoa fursa ya kuchagua wanamichezo
watakaowakilisha mikoa hiyo katika Mashindano Hayo ngazi ya Taifa Kibaha Mkoani
Pwani, Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara, Hipson Kipenya amesisitiza wanamichezo wote
kucheza na kushindana bila kuumizana na kucheza kwa upendo na kuzingatia
nidhamu kama ambavyo Wakiwa mashuleni kwao na kuwataka wanamichezo hao kurudi
na ushindi ili kujenga Heshima ya Mikoa hiyo kimichezo.
Wakielezea mategemeo ya kuchaguliwa wanafunzi zaidi wenye vipaji kutoka Mikoa Hiyo kutokana na walivyojiandaaa,Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Masasi mkoani Mtwara na Afisa Elimu SekondariManispaa ya Lindi walitoa ombi kwa Wizara.
0 comments:
Post a Comment