Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo meneja wa bia ya Kilimanjaro ambayo ndiyo wadhamini wakuu wa tuzo hizo George Kavishe amesema mwaka huu kumekuwa na mwitikio mkubwa zaidi kwa wadau wa muziki kupigia kura wasanii wanaowania tuzo hizo katika makundi 37, zoezi ambalo lilifungwa May 31 na kwamba kwa sasa wasanii mbalimbali wapo kambini kwa ajili ya maandalizi ya kutoa burudani kabambe kwenye sherehe hizo zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam.
GEORGE KAVISHE - Meneja - Bia ya Kilimanjaro |
Kavishe amesema kuwa
wadhamini wa tuzo hizo mwaka huu zinazobeba ujumbe wa KIWETUKWETU wameandaa
vituo maalum vya wazi katika maeneo ya Mabatini Mwanza, uwanja wa CCM - Moshi
na nje ya uwanja wa taifa - Dar es salaam kwa ajili ya wananchi ambao
hawatapata fursa kwenda Mlimani City kushuhudia sherehe hizo zitakazoonyeshwa
moja kwa moja na televisheni.
Gharama za tiketi hizo
zitakazouzwa katika maeneo ya Mlimani City, Boorn to shine mwenge, Roby One
Fashion kinondoni na Sharks Limited mtoni kwa Aziz Ali ni shilingi 75,000 kwa
wageni maalum yaani VIP, na shilingi 20000 kwa wageni wa kawaida.
0 comments:
Post a Comment