Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku huu itakuwa na kibarua
kigumu dhidi ya wenyeji wao Ivory Coast katika mchezo wa awali wa michuano ya
kufuzu kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Kikosi hicho ambacho kinanolewa na kocha Kim Poulsen kitaingia
Uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa Kimataifa
wa kirafiki mwaka 2010.
Poulsen anaamini kuwa wachezaji wake hawatatishwa na majina
makubwa ya wachezaji wa Ivory Coast hususan wanaocheza katika ligi ya Uingereza
na kwamba tayari amewaandaa kisaikolojia.
|
Mbwana Samatta |
Taifa Stars katika mchezo huo itaongozwa na mshambualiji wake
Mbwana Samatta, anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC pamoja na John Bocco wa timu ya Azam FC.
|
John Bocco |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment