Nchini Kenya matukio ya milipuko yanaendelea ambapo mjini Mombasa
mlipuko mkubwa umetokea karibu na kituo kimoja cha kuuzia mafuta.
Kwa mujibu wa mashuhuda watu watatu waliokuwa kwenye gari
walirusha kitu kuelekea kwenye kituo hicho kwa lengo la kukilipua, lakini
ilishindikana kutokana na umbali wa mahali waliporushia ambapo habari zinasema
tukio hilo ni muendelezo wa mashambuliziyanayofanywa na wafuasi wa kundi la
al-Shaabab.
Polisi mjini Mombasa wametangaza msako dhidi ya watu hao ingawa
baadhi ya wakazi wamelalamikia walichodai ulinzi duni.
0 comments:
Post a Comment