Wakati Ivory Coast wakiwasili nchini Jeshi la
polisi kanda maalum Dar es Salaam limesema limejipanga katika kuimarisha ulinzi
na usalama katika mechi kati ya taifa stars na ivory cost inatarajiwa kufanyika
siku ya jumapili katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa polisi kanda maalum ambaye ni
mwenyekiti wa kamati ya usalama wa uwanja huo amesema ni marufuku kwa mtu
yeyote kuingia na silaha zikiwemo zile za moto au visu na magari yote
yataegeshwa nje ya uwanja huku magari ya kazi maalum na viongozi tu ndiyo
yataruhusiwa kuingia uwanjani hapo.
![]() |
| Suleiman kova - Kamishna wa jeshi la polisi kanda maalum DSM. |
Aidha jeshi hilo limewatahadharisha mashabiki
kuzingatia sheria na kufuata taratibu zinazokubalika uwanjani hapo kwa kuwa
tayari hatua za kiusalama za kubaini wakorofi zimechukuliwa baada ya kuweka
kamera za usalama kila kona ya uwanja huo wa taifa.

(2).jpg)
0 comments:
Post a Comment