Timu ya soka ya Ivory Coast imewasili nchini
jana usiku kwa tayari kwa mchezo dhidi Taifa Stars kwa ajili ya kusaka tiketi
ya kushiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil Mwakani.
Timu hiyo imewasili ikiwa ni nyota wake
kadhaa akiwemo kiungo wa Manchester City Yaya Toure,Gervihno wa Arsenal,Tiote
wa New Castle,Solomon Kalou anayesakata soka nchini Ufaransa na Arouna Kone.
Timu hiyo imewasili bila nyota wake Didier
Drogba anayechezea Galatasaray ya Uturuki.
Wakati Timu hiyo Stars ambayo imeweka kambi
kwenye hoteli ya Tansoma imendelea na mazoezi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar
es Salaam kujiandaa na mchezo huo utakaofanyika Jumapili.
Wakati huo huo makocha wa timu zote mbili
watakutana na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya shirikisho la soka
nchini (TFF) kwa ajili ya kuzungumzia jinsi walivyojiandaa kwa mechi hiyo.


0 comments:
Post a Comment