Na. Kuringe Mongi, Dodoma.
Hatimaye Serikali imetoa msimamo mpya wa kuziruhusu
timu za Yanga Simba na Super Falcons ya Zanzibar kushiriki kwenye michuano ya
Kombe la Kagame nchini Sudan baada ya kuhakikishiwa na Serikali ya nchi hiyo
kwamba itatoa ulinzi wa kutosha kwa ya timu za Tanzania.
Naibu Waziri Habari
Vijana Utamaduni na Michezo Amos Makalla akizungumza na Waandishi wa
Habari Mkoani Dodoma amesema kwamba wameandikiwa barua na serikali ya Sudan
ikiwahakikishia kwamba timu za Tanzania zitapewa ulinzi mkubwa zisiweze
kudhurika na machafuko yanayoendelea
Sudan.
![]() |
| Amos Makalla - Naibu waziri wa Habari Vijana Utamaduni na michezo. |
Amesema licha ya serikali kuja na msimamo mpya bado ni
jukumu la timu hizo kuamua kwenda au kutokwenda Sudan kwa ajili ya Michuano
hiyo ya Afrika Mashariki na Kati inayotarajiwa kuanza juni 18 mwaka huu.
Tamko hilo na serikali limekuja siku chache baada ya
Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Mkenya
Nicholas Musonye kutoa tishio la
kuzichukulia hatua kali dhidi ya timu hizo za Tanzania endapo hazitakwenda
kushiriki kwenye michuano hiyo mjini Khatoum.
Yanga wamepangwa Kundi C katika michuano hiyo pamoja
na Ports ya Djibouti, Express ya Uganda na Vital 'O' ya Burundi, wakati
wapinzani wao wa jadi, Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na wenyeji
El-Mereikh, Elman ya Somalia na APR ya
Rwanda.
Awali
Serikali ilitoa tamko la kuzuia
klabu za Tanzania kutokwenda Sudan kutokana na machafuko yanayoendelea nchini
humo.


0 comments:
Post a Comment