Na .Kuringe Mongi, Dodoma.
Waziri mkuu Bw. Mizengo Pinda ametoa wito kwa wabunge kupambana na rushwa (APNAC) tawi la Tanzania, kuingalia upya sheria ya rushwa na kuifanyia marekebisho, ili Taasisi ya kudhibiti na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Waziri Mkuu ameitoa rai hiyo mjini Dodoma, wakati
alipokuwa akifungua mkutano wa (APNAC) tawi la Tanzania, na kuweka wazi juu ya
malalamiko yanayohusu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwa na mamlaka ya mwisho ya
kesi za rushwa nchini.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wabunge hao ambao ni
wanachama wa (APNAC) kuipinga rushwa kwa nguvu zote, kwani hata vitabu
vitakatifu, vimekuwa vikionya juu ya rushwa.
Naye, Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania, Bibi Anne Makinda akimkaribisha waziri mkuu kufungua mkutano huo,
hakusita kuwataka wabunge kuwa na nia ya dhati kukataa kuchukua rushwa, kama
kweli wanataka kuisimamia serikali.
![]() |
| Anne Makinda - Spika wa Bunge la Tanzania. |








0 comments:
Post a Comment