Msanii wa
maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania wa miondoka ya Hip Hop Langa Tottym Kileo maarufu
kama Langa aliyefariki jana kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili anatarajiwa
kuzikwa Jumatatu kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Taratibu za
mazishi zimekuwa zikiendelea kufanyika nyumbani kwa msanii huyo mtaa wa Ludi
Mikocheni Jijini Dar es Salaam ambako baadhi ya ndugu na jamaa na wasanii wenzake walikukusanyika kwa ajili ya kuomboleza msiba huo.
![]() |
| Marehemu Langa Tottym Kileo enzi za uhai wake. |
Wakizungumzia
jinsi walivyo pokea kifo cha msanii huyo,
wasanii Kala Jeremiah na Mukhi Edwards
wamesema kwamba ni pigo jingine kwenye tasni ya muziki wa hip hop nchini na
kwamba kifo chake hakitasahaulika.
![]() |
| Kala Jeremiah - Mwanamuziki wa Hip hop Tanzania |
Langa
alitambulika kwenye mashindano
yaliyofanyika mwaka 2004 ya Coca-Cola Pop Star yaliyofanyika Afrika Kusini kwa
kujumuisha nchi tatu za Afrika Mashariki ambapo enzi za uhai wake mwanamuziki
huyo alitamba na vibao kama Kiswanglishi,unanicha hoi.matawi ya juu akiwa na
kundi maarufu la Wakilisha la jijini Dar es Salaam na nyimbo nyingine nyingi.
Langa alizaliwa
desemba 23 mwaka 1985 na amekutwa na
umauti wakati akiwa anaumwa malaria wakati akipatiwa matibabu katika hospitali
ya rufaa muhimbili ambapo hapo ndipo
ikawa safari yake ya mwisho kimuziki.
Mungu ailaze
roho ya marehemu mahala pema Amen



0 comments:
Post a Comment