Na Khamis Suleiman, Dar Es Salaam.
Halmashauri ya manispaa ya Temeke leo imkifungia
kiwanda cha kinachotengeneza nywele Bandia maarufu kama wigi kutokana na
mazingira hatari ya kiafya na kiusalama huku kikiwa na wafanyakazi zaidi ya mia
330.
|
Wananchi wakiwa wanaangalia Hali ya ufungaji wa
kiwanda Hicho ukiendelea.
Kufungwa kwa kiwanda hicho cha Tanzania Hair
Industries kilichopo barabara ya Nyerere kunadaiwa kutokana na kutotekeleza amri
ya manispaa hiyo iliyolewa na mwanzoni mwa mwezi huu ambapo walitakiwa
kusimamisha uzalishaji kutokana na mazingira ya kazi hatarishi.
|
|
Baadhi ya wananchi waeneo hilo wakishangilia kufungwa
kwa Kiwanda hicho.
Miongoni mwa mazingira hayo hatarishi ni kuwapo kwa
matundu mawili tu ya vyoo kwa matumizi ya wafanyakazi 330, kutumia maji ya
kunywa ya bomba yasiokuwa salama, kutumika mlango mmoja tu wa kutoka hali
inayoweza kuleta maafa pindi itakapotokea moto
|
Afisa afya na mazingira wa manispaa ya temeke WILLIUM
MUHEMU ametaja sababu nyingine kuwa ni wafanyakazi kutokuwa na vifaa vya kinga,
sare za kazi, na kufungiwa na kufungua ambao mtu mmoja tu anashika ufunguo hali
ambayo ni hatarishi wakati wa dharura.
|
Willium Muhemu - Afisa afya na Mazingira wa Manispaa ya Temeke.Mara baada ya kuwasili eneo hilo Maafisa hao wa
manispaa walizuiliwa kuingia na walinzi eneo hilo ambapo baada baada ya kufungua wafanyakazi walitakiwa
kutoka nje na kuondoka. |
|
Walinzi wa kiwanda Hicho wakoneklana wakiwa kazini na
kuwazuia Maofisa Hao kufanya kazi yao
Kutokana na msongamano ulikuwapo zaidi ya wafanyakazi
kumi walipoteza fahamu.
|
|
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa wameanguka chini baada ya kupoteza fahamu. |
Viongozi wa kiwanda hicho akiwepo mkurugenzi wake
bw,Hussein Somania amekamatwa na anatarajia kufikishwa mahakamani.
|
Hussein Somania - Mkurugenzi wa Kiwanda Hicho. |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment