Image
Image

EXCLUSIVE: MISA TANI NA MCT : SERIKALI YAKUMBUSHWA HAKI ZA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.



Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN) na Baraza la Habari tanzania (MCT) imezikumbusha serikali za Afrika Mashariki kuendeleza haki na uhuru wa vyombo habari ikiwa ni utekelezaji wa tamko la ulimwengu la haki za binadamu na kulinda misingi ya utawala wa sheria wa kidemokrasia kwenye ukanda huo.

Aidha vyombo hivyo vimesema kwamba ni wajibu wa serikali hizo kuhakikisha kwamba kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni au kujieleza pamoja na kupata habari bila ya kuingiliwa.


Mwenyekiti wa MISA-TAN, Mohammed Tibainyendera na Meneja Maadili na Usuluhishi wa MCT Allan Lawa wakizungumza kwenye uzinduzi wa Tamko la Mount Meru juu ya uhuru wa vyombo habari, pia wamehimiza umuhimu wa uboreshaji wa maslahi ya waandishi wa habari pamoja na kuwahakikishia mazingira bora na salama katika utekelezaji wa majukumu yao kila siku.

Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) Francis Stolla akizungumza mara baada ya kuzindua tamko hilo la wanahabari ameahidi kufanya kazi na waandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kisheria bila malipo.

Tamko hilo la Mount Meru ambalo lilitolewa siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kwa mwaka huu mkoani Arusha pamoja na mambo mengine limelaani vikali ongezeko la kuwashambulia kuumizwa na kuuawa kwa waandishi wa habari katika ukanda wa Afrika Mashariki.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment