Bunge la Afrika mashariki linatarajiwa kujadili
na kupitisha miswada miwili ya sheria ya kuwa na kiwango kimoja cha uzito wa
mizigo na kuwa na kituo kimoja cha ukaguzi katika mipaka ya nchi wanachama wa
jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam,
katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo la Afrika Mashariki, bi.
SHYROSE BHANJI, amesema kwa mara ya kwanza vikao vya bunge hilo vitaanza kuendeshwa
kwenye makao makuu ya jumuiya hiyo jijini Arusha, Agosti mwaka huu ambapo
miswada hiyo itajadiliwa na baadae marais wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo
watatia saini ili kuwa sheria kamili.
![]() |
| SHYROSE BHANJI |
Bi. Shyrose aliyekuwa ameongozana na mbunge Abdullah Mwinyi wamesema faida ya miswada
hiyo kwa nchi wanachama ni pamoja na kuwezesha nchi hizo kuwa na kiwango kimoja
cha uzito wa mizigo barabarani ili kudhibiti uharibifu wa miundombinu hiyo
pamoja na kuondoa urasimu na ucheleweshaji katika mipaka ya nchi hizo, hatua
ambayo itaongeza kasi ya ukuaji wa biashara baina ya nchi wanachama.


0 comments:
Post a Comment