Mamia ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga jana
wamejitokeza kwenye mazishi ya aliyekuwa mwakilishi wa kituo cha televisheni
cha Channel Ten na Magic Fm mkoani humo, Marehemu Charles Hilila aliyefariki
dunia usiku wa kuamkia June 19 mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
![]() |
| Marehemu Charles Hilila Enzi za Uhai Wake. |
Marehemu Charles Hilila aliyezaliwa September 15
mwaka 1964, amezikwa jana katika kijiji cha Tinde mkoani Shinyanga ambapo
katika ibada ya mazishi Padri Emmanuel Kakoro wa kanisa Katoliki Jimbo Kuu la
Shinyanga aliwakumbusha wanadamu kumrejea Mwenyezi mungu muda wote kutokana na
mema anayowatendea.
Katika mazishi hayo kampuni ya Afrika Media
Group, inayomiliki vituo vya televisheni vya Channel Ten, CTN, C2C, DTV na
Radio Magic Fm iliwakilishwa na mwandishi wake wa mkoani Mwanza bw. Henry
Kavirondo.
Nao baadhi ya waliomfahamu marehemu Charles
Hilila wakati wa uhai wake wakiwemo wakazi na wanahabari wa mkoa wa Shinyanga
walimuelezea kwa mtazamo tofauti.
Marehemu Charles Hilila ambaye tulimpenda lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi
ameacha mjane na watoto watatu.......
Mungu ailaze roho ya marehemu Charles
Hilila mahala pema Amina.


0 comments:
Post a Comment