 |
Tatu Juma
Msichana Tatu Juma, mwenye umri wa miaka 21 mkazi
wa jijijni dar es salaam ambae amekatwa mikono yake yote miwili kutokana na
ajali ya gari anaomba msaada wa kifedha kutoka kwa wasamalia wema ili aweze
kununua mikono bandia itakayomwezesha kujihudumia mahitaji yake ya msingi.
|
 |
| Tatu Juma ndivyo anavyoonekana hali yakuwa mikono yake ikiwa imekatika. |
Akizungumza kwenye ofisi za channel ten ambako
alifuatana na mlezi wake, binti huyu Tatu ambae alimaliza kidato cha nne katika
shule ya sekondari Kileo moshi mwaka 2010 na kupata ajali ya gari ya daladala
jijini dar es salaam mwaka 2012 ambapo alikatika mkono mmoja hapo hapo na mwingine
walimalizia hospitali ya mifupa MOI kutokana na kupondeka kabisa.
Binti huyu anasema
kutokana na ulemavu alioupata wa kupoteza mikono yake yote miwili hawezi hata kufanya kitu chochote, hivyo kulazimu kutegemea ndugu zake wamsaidie.
 |
Tatu Juma ( kulia) akiwa na mlezi wake Hawa Msuya kwenye ofisi za Channel Ten. Amesema wamepata hospitali nchini afrika ya
kusini ambayo wanaweza kumpatia mikono itakayomwezesha kujihudumia mambo ya
msingi na kufanya vitu vidogo vidogo,
ambapo gharama za kikono peke yake ni sh million arobaini na tano, wakijumlisha
nauli za watu wawili na gharama nyingine inafika sh million sitini fedha za
kitanzania ambazo yeye na familia yake hawana uwezo wa kuzipata, hivyo
amewaomba watanzania ambao wataguswa na tatizo lake kumsaidia. ili aweze kupata
mikono hiyo ya bandia. Kwa yeyote atakayeguswa na matatizo ya Tatu na
kutaka kuchangia matibabu yake ya kupata mikono ya bandia anaweza kuwasiliana
nae kwa namba ya simu 0713 466721, au 0767 768 785 au 0715 501 223, na anaishi
jijini dar es salaam. |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment