Msanii maarufu wa
mashairi nchini Mrisho Mpoto pamoja na kundi lake la Mpoto Theatre Gallery
Limited, likiwa na jumla ya wasanii 28 anatarajiwa kuanza kampeni ya siku 45 ya
uhamasishaji wa usafi wa vyoo,mazingira na mikono katika mikoa mitano ya
Tanzania Bara juni 20.
Akizungumzia kampeni
hiyo inayolenga nchi nzima ikianzia
mikoa ya Dodoma,Mara,Njombe,Rukwa na Tanga.
Mpoto,amewaambia waandishi wa
habari Jijini Dar Es Salaam kuwa msanii wa vichekesho King Majuto atakuwemo pia
katika kampeni hiyo yenye lengo la kutoa elimu kwa jamii hususani ya vijijini,
namna wanavyoweza kuepuka maradhi hasa ya tumbo yatokanayo na matumizi yasiyo
sahihi ya vyoo na kutonawa mikono kwa hatua stahiki.
Awali Afisa mazingira kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii,Mariamu Mahmoud,alisema,kampeni hiyo ni muendelezo wa kampenu ya kitaifa zinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Juni 5 Mjini Moshi akati wa kilele cha siku ya usafi wa mazingira duniani.
Kwa Mujibu wa takwimu
za kitaifa,asilimia 91 ya wananchi wa vijijini hawana elimu juu ya matumizi
sahihi ya vyoo bora na unawaji stahiki wa mikono hali inayochangia vifo
vitokanavyo na maradhi ya tumbo


0 comments:
Post a Comment