Kufuatia uhaba wa chakula
hukoBurkina Fasomwaka 2012, shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa,
WFP nchini humo limeanzisha mradi mpya wa kuchagiza jamii kuibuka katika
mgogoro huo wa chakula na hatimaye kuweza kukabiliana na halikamahiyo baadaye
iwapo itatokea huku pia ikipunguza utapiamlo.
Burkina
Faso imeshuhudia mavuno mazuri mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Mavuno ya nafaka kutoka mwaka 2012 na 2013 yaliongezeka kwa asilimia 30
yakilinganishwa na ya mwaka 2011 na 2012.
Kutokana na hali ya
kiangazi iliyoshuhudiwa kati ya mwaka 2011 na 2012 bado taifa hilo
halijajikwamua kutoka kwenye janga la njaa huku watu milioni 1.8 nchini
Burikana Faso wakikabiliwa na uhaba wa chakula.
Familia nyingi zinakabiliwa na
changamoto za kupata chakula .
Mwaka 2012 viwango vya utapiamlo
vilipita vile vinavyowekwa na Shirika la afya dunianii WHO huku viwango vya
watoto wasiokua vikifikia asilimia 33.
Kwa sasa shirika la mpango wa chakula
duniani WFP limeanzisha oparesheni ya kukabiliana na utapiamlo kwenye maeneo
yaliyoathiriwa zaidi.
Opareshini hiyo itaendeshwa kwenye maeneo 10 kati ya
maeneo 13 ambapo itatoa chakula maalum na tiba kwa watoto walio kati ya
miezi 6 na 59 walio na utapiamlo.
0 comments:
Post a Comment