Nchini Madagascar baa la nzige ambalo udhibiti wake
unatia mashaka linaripotiwa kutishia usalama na uhakika wa chakula nchini humo
kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kama anavyoripoti Jason
Nyakundi.
FAO inakadiria kuwa
ifikapo mwezi Septemba mwaka huu karibu theluthi moja ya taifa
laMadagascar itakuwa imevamiwa na nzige na kuyaweka kwenye hatari karibu
maisha ya watu milioni 13 au karibu asilimia 60 ya watu wote wa nchi hiyo.
FAO imefanya hitihada
za kuchangisha dola milioni 22 kugharamia hatua za dharura za kukabilina
na nzige lakini hata hivyo kampeni hiyo haijaiungwa mkono kikamilifu
ikiwa inakabiliwa na uhaba wa fedha.
Mkurugenzi wa FAO Jose Graziano da Solva
anasema kuwa iwapo nzige hao hawatadhibitiwa huenda athari zao zikawa za
miaka mingi na pia watakuwa vigumu kuwazuia na kwa gharama ya juu.
Kulingana na tathmini iliyofanywa na
FAO ni kuwa maeneo fulani yaMadagascartayari yamepoteza kati ya asilimia 40 na
70 ya mchele na mahindi.
FAO inakadiria kuwa huenda karibu tani 630 za chakula
zikapotea au karibu asilimia 25 ya mahitaji yote ya nafaka
nchiniMadagascarsuala ambalo litaaathiri usalama wa chakula na pato la wengi.
0 comments:
Post a Comment