Serikali leo imewasilisha bungeni Muswaada wa
marekebisho ya sheria ya fedha kwa mwaka 2013 unaolenga kupunguza misamaha ya
kodi kwa wawekezaji na hatimaye kurekebisha viwango vya kodi kwenye mishahara
ya wafanyakazi.
Muswaada huo umewasilishwa punde tu na Waziri wa
Fedha Dk. William Mgimwa wakati akisoma
Muswaada huo wa sheria ya fedha kwa mwaka 2013 katika kikao cha Bunge la
Bajeti kwa mnwaka 2013/ 2014 Mjini Dodoma.
Mgimwa amesema kuwa marekebisho ya sheria hiyo
yatasaidia Kurekebisha sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 ili kupunguza
urasimu kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kwenye miradi ya maendeleo inayolenga
kuongeza mapato ya serikali na Kupunguza umasikini.
Hata hivyo
kwa mujibu wa waziri Mgimwa amesema chini ya muswaada huo sheria ya kodi ya
mapato itafanyiwa marekebisho ili kuchochea ushiriki wa sekta Binafsi kwenye
ujenzi wa uchumi wa Taifa pamoja na mambo mengine.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa muswaada huo lengo
lake kuu unazitaka pia taasisi au mashirika yanayomilikiwa na serikali
kuwasilisha asilimia 10 ya mapato ya mwaka kwenye mfuko mkuu wa serikali tofauti
na sasa ambapo waziri mwenye mamlaka amepewa dhamana ya kuamua kiwango cha
mchango wa taasisi hizo kwenye mfuko mkuu wa serikali.
0 comments:
Post a Comment