Hali ya rais wa zamani wa Afrika kusini Mzee Nelson Mandela imeripotiwa kuzidi kuzorota katika saa 48 zilizopita hatua iliyomlazimu rais Jacob Zuma wa nchi hiyo kufuta ziara yake ya kwenda Msumbiji ambako alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa marais uliokuwa umepangwa kufanyika leo.
Nelson Mandela - rais wa zamani wa Afrika kusini |
Habari kutoka nchini Afrika Kusini zinasema, rais
Zuma amefikia uamuzi huo baada ya kumtembelea Mzee Mandela kwenye hospitali
alikolazwa kwa ajili ya matibabu na kuelezwa na madaktari wanaomhudumia kwamba
hali yake imezidi kuzorota hali inayozua taharuki zaidi nchini humo.
Jacob Zuma - Rais wa Afrika Kusini |
Watu mbalimbali wameendelea kukusanyika nje ya
hospitali alikolazwa Mzee Mandela wakiwa na ujumbe wa kumtakia heri kiongozi
huyo anayeheshimika duniani na kwa mujibu wa wadadisi wananchi wa Afrika Kusini
wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu hali ya Mandela.
0 comments:
Post a Comment