Na Charles Hilila,Shinyanga.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi iliyopo manispaa ya
Shinyanga wamepongeza juhudi za wadau wa elimu mkoani humo kuipatia nishati ya
umeme shule hiyo.
Wamesema kuwa, kupatikana kwa nishati hiyo kutasaidia kuinua
kiwango cha taaluma shuleni hapo na kufanya majaribio kwa vitendo kwa wanafunzi
katika masomo ya sayansi ambapo awali walikuwa wanafanya kwa nadharia kutokana
na kukosekana kwa umeme.
Akizindua matumizi ya nishati hiyo shuleni hapo, mkurugenzi
mtendaji wa Bank ya Posta nchini Bw. Tabasama Moshindi ambaye alichangia
milioni 1.2 kwa ajili ya kutandaza nyaya katika madarasa na nyumba za walimu
amewaasa vijana hao kutumia umeme huo kwa kuongeza maarifa na kujisomea ili
waweze kufaulu mitihani yao .
Kupatikana kwa umeme huo shuleni hapo kutasaidia kuchochea mwamko
wa elimu na ari ya kujifunza kwa wanafunzi hao hata nyakati za usiku na kuinua
viwango vya taaluma
0 comments:
Post a Comment