Rais wa Marekani Barack Obama ameanza ziara yake
barani Afrika ambapo anatarajiwa kuzuru nchi tatu.
Hata hivyo ziara hiyo imeghubikwa na wingu la mustakabali
wa afya ya kiongozi wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ambaye bado yuko
hospitalini katika hali mbaya akihudumiwa na jopo la madaktari. Afrika kusini
ni miongoni mwa nchi zitakazotembelewa na Rais Obama katika ziara hiyo ya wiki
moja. Nchi nyingine ni Senegal na Tanzania.
Ikulu ya Marekani imesema itashauriana na familia ya
Bwana Mandela kuona ikiwa Rais Obama anaweza kumtembelea mwanasiasa huyo
mkongwe aliyelazwa katika hospitali ya mjini Pretoria kwa muda wa wiki tatu
sasa.
Bwana Mandela na Obama hawajawahi kukutana ana kwa ana
tangu Rais huyo wa Marekani alipochaguliwa kuingia madarakani kwa mara ya
kwanza mwaka 2008.
0 comments:
Post a Comment