Mmiliki wa klabu ya Chelsea
Roman Abramovich akitimiza miaka kumi ya umiliki wake darajani na kupondwa na
baadhi ya makocha kwa sera yake ya kutumia fedha nyingi kununua wachezaji nje
ya England na kuwanyima wazawa nafasi ya kucheza, sasa bilionea huyo mwenye
kiburi cha pesa amesema anahitaji kuona maendeleo makubwa katika kituo cha
kulelea vipaji cha klabu hiyo (Chelesea Academy) ili kuijenga upya timu Hiyo.
![]() |
|
Abramovich, kulia, akishangilia na
Frank Lampard, katikati, na John Terry, kushoto, mnamo mwaka
2005
|
![]() |
|
Terry enzi za ujana wake katika klabu ya
Chelsea career
|
![]() |
|
Roman Abramovich anataka wachezaji
vijana zaidi kutoka katika Akademi yake ya Chelsea.
|
Kwa mujibu wa mtandao
Sportsmail.com ulioeinasa kauli ya bilionea huyo kuwa anahitaji kuzalisha
wachezaji wa kwake siku zijazo ili kuwarithi wakongwe wa klabu hiyo.
Wapo wachezaji
wakongwe kama vile nahodha John Terry na Frank Lampard – ambao
walisainishwa mwaka 2001 kutoka West Ham,
Ambapo hadi wakati huu wanaonekana kuwa ni nguzo muhimu ndani ya klabu.
![]() |
|
Nyota wa Chelsea Ryan Bertrand, akiwa na
meneja wake Jose Mourinho katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpia.
|
Aidha Abramovicha amedai anatakiwa kuzalisha wachezaji wapya
kutoka katika Akademi yake na kuachana na hasara kubwa anayoipata kwa kununua
wachezaji wa bei kubwa.






0 comments:
Post a Comment