Mwanariadha
mashuhuri wa Ethiopia Haile Gebrselassie ametangaza kujiunga na siasa kwa
matumaini ya kushinda ubunge hapo mwaka wa 2015.
Tangazo
hilo linatokana na kuwa kuna na kwamba nyota huyo wa Olimpiki anapanga kustaafu
kutoka riadha.
Haile ni mshindi mara mbili wa mbio za 10,000 katika michezo ya
Olimpiki na anashabikiwa na wengi nchini Ethiopia.
Hata hivyo hajatangaza chama
cha kisiasa ambacho atatumia kuwania ubunge.
Kwa miaka
mingi bunge la Ethiopia limethibitiwa na wabunge wa chama tawala cha People's
Revolutionary Democratic Front (EPRDF). Kuna mbunge mmoja pekee wa upinzani.
Akijibu
mashabiki wake kupitia Twitter, Haile alisema ni kweli kwamba ananuia kujiunga
na siasa mwaka wa 2015.
Alitanagaza kustaafu mwaka wa 2010 lakini akarejea tena
uwanjani na mwezi Aprili alishinda mbio za nyika za Vienna.
Pia alishiriki Marathon ya Boston iliyokumbwa na shambulio la bomu
ambapo watu watatu walikufa na makumi kujeruhiwa.


0 comments:
Post a Comment