Chadema Cha democrasia na maendeleo chadema kimepinga
kauli ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuhusu
hatima ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 kikisema mchakato wa sasa wa Mabaraza ya
Katiba, usiwe kikwazo cha mjadala wa muundo wa Serikali Tatu.
Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika alisema Dar es Salaam jana kuwa hatima ya
Uchaguzi Mkuu wa 2015 utakaotokana na mchakato wa mabadiliko ya Katiba
unaoendelea, siyo suala la kusubiri.
Akizungumza na Tambarare halisi kuhusu kauli ya Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe
kwamba endapo mapendekezo ya Serikali Tatu yatapitishwa, kuna hatihati ya
Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika, Jaji Warioba alisema:
“Tuachieni muda… hayo
mengine ni hisia tu. Ni kweli tunayajua lakini acheni tumalize hili kwanza ( la
Mabaraza ya Katiba). Hii ndiyo hatua tuliyopo sasa.”
Lakini jana Mnyika
alisema: “Hatuwezi kusubiri hadi Mabaraza ya Katiba yakamilishe mchakato kama
alivyoeleza Jaji Warioba katika gazeti la Mwananchi toleo la leo, (jana),”
alisema Mnyika kwa simu.
Jaji
Warioba alitaka suala la muundo wa Serikali Tatu utakavyokuwa lisiwe hoja kwa
sasa kwa kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inachokifanya ni kukusanya maoni
kupitia Mabaraza ya Katiba na kisha kuandaa rasimu itakayopelekwa bungeni kwa
ajili ya majadiliano na kwamba mjadala huo utawachanganya wananchi endapo
utaingizwa katika hatua hii ya ukusanyaji maoni.
Mnyika
alisema: “Mijadala hii haiwezi kusubiri mpaka hatua ya Mabaraza ya Katiba,
inapaswa kuanza wakati huu kupitia mabaraza yanayosimamiwa na Tume na Mabaraza
yanayoendeshwa na makundi ya kijamii.
“Pia, masuala hayo ya mpito pamoja na
marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ni mambo ambayo yanapaswa
kutolewa ufafanuzi wa ziada na Serikali zaidi ya kauli ambayo Waziri wa Sheria
na Katiba Mathias Chikawe ameitoa kupitia gazeti la lenu la leo (jana).”
Alisema kimsingi
bado kunahitajika mjadala wa masuala ya mpito kwa sababu kuna uwezekano kwamba
Katiba Mpya, ya Muungano au ya Zanzibar na ya Tanganyika, isiwe tayari kabla ya
Uchaguzi Mkuu wa 2015, endapo suala la Serikali tatu litapita.
Alisema kwa upande
mwingine, rasimu ya Katiba iliyotolewa imeibua mjadala juu ya mkwamo wa
kikatiba (constitutional stalemate), ambao ni muhimu upatiwe suluhisho akisema
chama chake kinapendekeza mchakato wa Katiba Mpya ya Tanganyika uanze mara moja
ili uende sambamba na huu wa Katiba Mpya ya Muungano.
Alisema ilikuwa vyema
yote yakajadiliwa katika Bunge la Agosti 27, mwaka huu.
Waziri Chikawe
alikaririwa na gazeti hili juzi akisema: “Uwepo wa Serikali tatu utafumua mfumo
mzima wa utendaji ndani ya Serikali.
Hatuwezi tena kufanya uchaguzi wa Rais na
wabunge 2015, hatuwezi kufanya chochote nje ya Katiba ya Serikali Tatu kwa kuwa
kinachofuata ni kuunda Katiba nyingine inayohusiana na Serikali tatu.
Waziri Chikawe afafanua
Juzi, Waziri Chikawe
alitoa ufafanuzi juu ya utata wa hoja zake kwa kuipongeza Tume ya Jaji Warioba
kwa kazi inayofanya huku akisema anaunga mkono msimamo wa CCM wa kutaka
kuendelea na muundo wa Muungano wa Serikali mbili.
Aidha Alisemamchakato wa
kuandika Katiba Mpya unapaswa kuangaliwa kwa jicho pana zaidi ya lile la
Uchaguzi Mkuu wa 2015.
0 comments:
Post a Comment