Mathias Chikawe
Waziri wa Katiba na Sheria nchini
Tanzania, Mathias Chikawe, amesema kama Watanzania watakubali muundo wa
serikali tatu uliopendekezwa katika Rasimu ya Katiba Mpya, kutahitajika
mabadiliko makubwa ya kisheria na kitaasisi ili kuwa na sheria nzuri zitakazodhamini
uchaguzi huru na wa haki mwaka 2015.
Kiongozi huyo amekanusha tuhuma
alizoelekezewa na vyombo vya habari kwamba anao ushahidi unaoonyesha kuwa
serikali ya Rais Kikwete inapanga kuchelewesha uchaguzi ujao.
Amesema muundo wa
serikali tatu ukikubaliwa utahitaji muda wa maandalizi ingawa hiyo haina maana
kwamba uchaguzi usongezwe mbele.
Waziri Chikawe ametahadharisha juu ya muundo wa serikali 3 na kuwataka Watanzania watathmini kwa makini matokeo yake,
changamoto, gharama na natija ya muundo huo kabla ya kuchukua maamuzi yoyote.
0 comments:
Post a Comment