Waandamanaji wanaomuunga mkono rais Muhammad Mursi.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya mpito ya Misri, Mohammad Ibrahim
amesema kuwa, maafisa wa usalama wanajiandaa kuwatawanya waandamanaji wanaomuunga
mkono rais aliyepinduliwa, Muhammad Mursi.
Ibrahim amesema vyombo vya usalama
vitafanya hivyo kwa mujibu wa sheria na kwamba mikakati imewekwa ili
kuhakikisha hakuna umwagikaji wa damu utakaotokea kwenye oparesheni hiyo.
Waziri huyo wa Mambo ya Ndani amesema wananchi walijitokeza kwa wingi siku ya
Ijumaa kwenye medani ya Tahrir wameipa serikali idhini na baraka ya kuwaondosha
kwa nguvu wafuasi wa Mursi.
Hii ni katika hali ambayo, wafuasi wa kiongozi huyo
aliyepinduliwa wameapa kuendelea kukaa nje ya msikiti wa Rabaa Al-Adawiya
katika mji wa Nasr ulioko viungani mwa Cairo hadi pale Dkt. Mursi
atakaporejeshwa madarakani.
0 comments:
Post a Comment