Cecile Kyenge
Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Italia limesema kwenye
ripoti yake kwamba, ubaguzi wa rangi barani Ulaya bado ni tatizo sugu.
Shirika
hilo linalojiita I CARE limesema tukio la hivi karibuni la kutupiwa ndizi
waziri wa kwanza mweusi nchini humo limedhihirisha kuwa, ubaguzi wa rangi
Italia na barani Ulaya kwa ujumla bado ni tatizo kubwa na lilanopaswa
kukabiliwa vikali.
Bi. Cecile Kyenge alitupiwa ndizi wakati akihutubia siku ya
Ijumaa katika mji wa Cervia mkoani Ravenna, tukio linalonasibishwa na nyani au
sokwe-mtu.
Hii si mara ya kwanza kwa waziri huyo kukumbana na hujuma hiyo ya
ubaguzi wa rangi. Miezi kadhaa iliyopita, Waziri Kyenge alizomewa na kundi la
vijana mashariki mwa nchi hiyo na baadhi yao pia kumtupia ndizi.
0 comments:
Post a Comment