Washauriwa kuwa watulivu vuguvugu la misri.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
imeelezea masikitiko yake kufuatia mauaji ya makumi ya watu katika machafuko ya
hivi karibuni Misri na kutoa wito kwa pande zote hasimu nchini humo kujitadhidi
kudumisha utulivu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Iran Abbas Araqchi ametoa kauli hiyo na kuongeza kuwa, Tehran ina matumaini
kuwa watu wa Misri watakuwa waangalifu na kutumia hekima ili kuvunja njama za
maadui wanaotaka kuvuruga mapinduzi yaliyojiri nchini humo mwaka 2011.
Araqchi
ametoa wito kwa vyama vya kisiasa na viongozi wa Misri kuheshimu mshikamano wa
kitaifa, haki za kimsingi za wananchi na misingi ya demokrasia ili kufungua
njia ya mazungumzo na maelewano ya kitaifa.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelaani
vikali ongezeko la machafuko nchini Misri.
Amevitaka vikosi vya usalama vya
nchi hiyo kuheshimu haki za binadamu kikamilifu katika vitendo vyao, zikiwemo
haki za kujieleza na kujumuika.
Ban ametaka tena Bwana Mohammed Morsi na
viongozi wengine wa chama cha Muslim Brotherhood ambao sasa wapo kizuizini
waachiliwe huru mara moja au kesi zao kuangaliwa kwa njia ya uwazi.
0 comments:
Post a Comment