Wapiga kura wakiwa wanaonekana hapo katika
Picha.
Raia wa Mali wanapiga kura
leo Jumapili(28.07.2013) na kupuuzia vitisho vya waasi wa Kiislamu na
kujitokeza kwa mamilioni kupiga kura kumchagua rais mpya ambaye anatarajiwa
kuanzisha enzi mpya ya amani na uthabiti.
Wapiga kura
watakuwa na fursa ya kuchagua miongoni mwa wagombea 27 wakati wakipiga kura kwa
mara ya kwanza tangu mapinduzi ya mwaka jana katika nchi hiyo ambayo ni moja
kati ya nchi za eneo hilo yenye demokrasia imara, baada ya wapiganaji wa
Kiislamu walipochukua fursa ya vuguvugu la kutaka kujitenga na kudhibiti eneo
kubwa la nchi hiyo upande wa kaskazini.
Uchaguzi
umeanza saa nne asubuhi saa za Mali chini ya ulinzi mkali baada ya moja ya
makundi ya Waislamu kaskazini ya Mali kusema jana Jumamosi (27.07.2013) kuwa litashambulia
vituo vya kupigia kura.
"Vituo vya
kupigia kura na maeneo mengine yatakayofanyika zoezi hilo la kupiga kura katika
kile wanachoita uchaguzi yatalengwa katika mashambulizi ya Mujahideen, "
kundi la vuguvugu la umoja na Jihad katika Afrika magharibi (MUJAO) limesema
katika taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la Mauritania ANI.
Taarifa hiyo
haikufafanua ni njia gani zitatumika katika mashambulizi hayo.
Kundi hilo
limewaonya Waislamu wa Mali kutoshiriki katika zoezi hilo la kupiga kura , likiwaamuru
"kujitenga na uchaguzi huo."
Licha ya kuwa
kampeni iliyochukua wiki tatu ilimalizika rasmi Ijumaa bila kutokea tukio
lolote baya , hali hiyo inasababisha kutanda kwa wingu la machafuko katika eneo
la kaskazini ambalo limekuwa na shaka ya kuwapo tayari kwa Mali kufanya
uchaguzi ambao utakuwa huru na wa haki na wenye kuaminika.
Wakosoaji wanasema.
Wakosoaji
nchini humo pamoja na nje ya nchi wamedai kuwa Mali, ikiwa chini ya mbinyo
kutoka kwa jumuiya ya kimataifa , inaharakisha kufanya uchaguzi huo na kuhatarisha
kuwa na uchaguzi ambao hautakamilika ambao unaweza kuleta madhara zaidi badala
ya hali bora.
Lakini Louis
Michel, mkuu wa kundi la uangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya, ameeleza
matumaini siku ya Ijumaa, akisema hali ni nzuri kwa ajili ya kufanyika duru ya
kwanza ya uchaguzi wa kuaminika.
"Naamini
kwamba uchaguzi huu unaweza kufanyika katika muktadha na masharti ambayo
yanakubalika na hayaruhusu hali ya kutoaminika ama udanganyifu wa
matokeo," amewaambia waandishi habari katika mji mkuu Bamako.
Wasi wasi
mkubwa kabla ya uchaguzi huo umekuwa ukielekezwa katika mji wa Kidal, uliokuwa
ukidhibitiwa kwa muda wa miezi mitano na Watuareg wanaotaka kujitenga hadi pale
makubaliano ya amani yaliporuhusu jeshi la Mali mapema mwezi huu kutoa huduma
za usalama katika mji huo.
Mapigano kati
ya Watuareg na raia weusi wenye asili ya Afrika kabla ya uchaguzi yamesababisha
vifo vya watu wanne . Na watu wenye silaha wanaofikiriwa kuwa ni kutoka la
National Movement for the Liberation of Azawad MNLA wamewateka nyara maafisa
watano wa tume ya uchaguzi kilometa 200 kaskazini mwa Kidal.
Uchaguzi wa kwanza.
Uchaguzi huo ni
wa kwanza tangu jeshi kuasi Machi mwaka uliopita ambapo aliangushwa kutoka
madarakani rais Amadou Toumani Toure ambaye alichaguliwa kidemokrasia. Mtafaruku
uliofuatia ulisaidia kundi la MNLA, MUJAO na makundi mengine yenye mafungamano
na al-Qaeda kulidhibiti eneo la kaskazini ya Mali.
Katika mkesha
wa uchaguzi , kaimu rais wa Mali Dioncounda Traore, katika hotuba aliyoitoa
kuptia televisheni , amewataka watu wa Mali kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa
wingi kupiga kura katika nchi hiyo ambayo watu wanaojitokeza kupiga kura kwa
kawaida huwa chini ya asilimia 40. Traore binafsi si mmoja kati ya wagombea.
Kwa msaada wa Reuters.
0 comments:
Post a Comment