Christian Benitez Enzi za uhai wake.
Mshambuliaji
wa Ecuador Christian Benitez amefariki dunia nchini Qatar siku ya jumatatu
akiwa na umri wa miaka 27. Shirikisho la soka nchini Ecuador limethibitisha
taarifa hiyo na kusema mchezaji huyo amefariki kutokana na maradhi ya shinikizo
la moyo.
Kituo
cha televisheni cha Gama cha nchini Equador, kimeripoti kuwa Benitez maarufu
kwa jina la “Chucho” alifikishwa hospitalini siku ya jumapili akikabiliwa na
maumivu ya tumbo na amefariki ghafla siku ya jumatatu baada ya kupatwa na
matatizo ya moyo.
Kifo
hicho kimewashtua wanachama wa klabu ya El-Jash ya Qatar aliyokaa nayo kwa
kipindi kifupi, Benitez alisajiliwa klabuni hapo Julai 6 mwaka huu na siku moja
kabla ya kifo chake alishuka dimbani na klabu hiyo iliyokuwa ikimenyana na
Qatar Sports Club.
Klabu
hiyo imetuma salamu za rambirambi kwa familia na mashabiki wa mchezaji huyo na
kusema Benitez hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya katika mechi hiyo ambayo
ilikuwa ni ya kwanza toka alipojiunga nayo.
Benitez
alijipatia jumla ya mabao manne katika jumla ya michezo 36 aliyoshuka dimbani
na kujipatia umaarufu katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2006 nchini
Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment