Munir Zakaria, Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amesema Serikali yake
inawakaribisha wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuwekeza katika sekta ya
uvuvi wa bahari kuu, ili iweze kubadilisha maisha ya wananchi wengi wa visiwani
humo.
Dk.Shein ametoa wito huo
alipokutana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Bw.Mark
Simmonds aliyemtembelea ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo ambayo
pia yamehudhuriwa na Balozi wa uingereza hapa nchini Bibi Diana Melrose,
Dk.Shein amesema jitihada za pamoja za kuimarisha ushirikiano katika biashara
na uwekezaji zitasaidia kuongeza kasi ya uchumi hapa nchini.
Dk.Shein amemueleza Waziri
huyo kuwa Serikali yake imedhamiria kukuza sekta ya uvuvi wa bahari kuu, ambayo
hadi hivi sasa haijapata wawekezaji, na kuelezea matumaini yake kuwa wawekezaji
kutoka Uingereza watachangamkia fursa hiyo kuwekeza visiwani hapa.
Aidha Dk.Shein ameishukuru
Serikali ya Uingereza kwa misaada yake kwa Tanzania, ambayo pia inainufaisha
Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake, Waziri Mark
Simmonds amesema dhamira ya Serikali ya uingereza ni kupanua maeneo mapya ya
ushirikiano katika Nyanja za biashara na uwekezaji.
Waziri Simmonds amesema
pamoja na Uingereza kuongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania, kuna umuhimu mkubwa
kwa nchi hiyo kuimarisha zaidi uwekezaji na biashara kwa faida ya serikali na
wananchi wa pande zote mbili.
Viongozi wengine waliohudhuria mazungumzo hayo
ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Dk.Mwinyihaji Makame na
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Abdulhamid Yahya
Mzee.
Katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo
kwa haraka, serikali imeamua kuupa kipaumbele kwa kuuingiza katika mpango wake
wa matokeo makubwa ya haraka sasa (Big Results Now), ambapo ujenzi wake
utachukua miezi kumi na minane na kukamilika mwaka 2014, ambapo utakuwa na
uwezo wa kusafirisha futi za ujazo 784 kwa siku bila mgandamizo na ukiwekwa
mgandamizo utasafirisha futi za ujazo 1002 kwa siku.



0 comments:
Post a Comment