Na. Esther Zelamula Dar Es Salaam
Washiriki Mbali mbali wa kiserikali wakiwa wapo kwenye ofisi za wama ambapo Michelle obama wakati akifanya mazungumzo na mama kikwete leo wakiwa wanafuatila.
|
Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama aliyeko nchini
akiambatana na mumewe kwa ziara ya siku mbili leo amekutana na kufanya
mazungumzo na mwenyeji wake mke wa rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete jijini
Dar es salaam.
Mama Salma Kikwete (Kulia) Akipiga picha ya Pamoja na Mke wa Rais Obama Michelle
obama kwenye ofisi za Wama leo jijini Dar es Salaam..
|
Mama Salma Kikwete (Kulia) Akisalimiana na Michelle
obama kwenye ofisi za Wama leo.
|
Mara baada ya kuzungumza na Mama Kikwete, Mama Obama
pia alipata fursa ya kutembelea Makumbusho ya taifa .
Mama Salma Kikwete (Kulia) Akiteta jambo na Michelle
obama kwenye ofisi za Wama Picha zote na (Semvua Msangi).
|
Hafla fupi ya kumkaribisha Mama Obama kwenye viwanja
vya WAMA, imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa
Umoja wa Mataifa UN Dk. Asha Rose Migiro, Mke wa rais Mstaafu Mama Anna Mkapa,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba na mke wa Waziri
Mkuu mama Tunu Pinda.
Ujio wa Rais Barack Obama wa Marekani na familia yake
hapa nchini, ni kielelezo tosha cha ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani
na ni fursa kwa wananchi na serikali yaTanzania katika jitihada za kuimarisha
na kukuza uchumi wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment